gsa entertainment
Friday, 12 October 2012
Dalili 7 Za Mwanamke Gold Digger
HIZI NI DALILI ZA MWANAMKE GOLD DIGGER....KAA HUMO,UKIONA UMEZIONA HIZI DALILI KWA MTU JIPANGE AU UKAE MGUU PANDE...MGUU SAWA
1. ANAOMBA UMNUNULIE KITU CHA BEI AU UMKOPE HELA NDEFU SIKU ZA MWANZO TU ZA UHUSIANO
Hii ni dalili kwamba Mahaba/Ngono anayokupa unailipia bila kujua.Hakutozi hela ukimaliza tendo lakini few hours later au baada ya siku 1 tu,utapigwa mzinga baab kubwa ambao kwa namna moja au nyingine unatoa picha kwamba ni TIT for TAT,Nimekupa utamu wangu na wewe lazima Wallet yako itikisike kulipia utamu huo.Umewahi kukumbana na hii?????Umekumbana na Gold Digger!
2. ANAVAA VITU VYA BEI MBAYA SANA,ANAMILIKI SIMU GHALI AMBAZO WEWE MWENYEWE HUNA NA HANA KAZI
Haya sasa....Unawajua type hii??Ukimuona swagger zake ni za bei...Nywele feki (Wigi) bei mbaya,Viatu bei mbaya....Simu za Bei ghali..Nguo ananunua kwenye maduka ambayo bei zake ni za hatari hatari....Ukimuuliza anafanya wapi kazi...HANA KAZI....HANA BIASHARA....Shes just at home,kwa wazazi....Na wazazi wenyewe wala sio wa kishua kusema wanampa all these stuffs....Dingi atoe laki7 ya Weaving....Milioni ya iPhone na BB Torch....Wazazi wa namna hii walikufa na Azimio La Arusha...SIDHANI! Sasa anapataje vitu na kuweza kuvimanage na yeye kumanage kuishi expensive wakati Life yake na ya familia ni Poor....Jiulize!Na watajitetea sana lakini Je, Wanaokota hizo hela???Mbona sie hatuokoti???
3. HATA SIKU MOJA HALIPI BILI NA HATA AKILIPIWA HASEMI ASANTE
Hapo chacha!Ni kweli kwamba siku ya kwanza wakati Mwanaume anakutokea lazima alipie misosi na nini...Si ndo amekuita kwenye Date????Hilo linaeleweka....Ila mshaenda Outing mara mia8....Zote anakausha...Ikifika mida ya Bili yuko bize na kujibu BBM,hataki hata kujua bili ni Sh ngapi maana vitu alivyokula ni vya bei na anajua bili ni maumivu tu....Atajifanya yuko bize,aidha meseji au anaongea na simu....Hapo jua ngoma inogile,Unguza tu wallet mwanangu....
4. ANATAKA KWENDA MIGAHAWA YA BEI TU,AU HOTELI ZA BEI GHALI KULALA NA KULA
Hawa pia wapo,tena wengi...Wao madai yao eti ni watu wa CLASS.....Ukimwambia mkale mahali atakutajia sehemu ambazo wewe hata hujawahi kuwaza kula.....Lets go to Saverios tukale Prawns...Kitu elfu 70....twende sijui Pub gani....Mara level 8 is a chilly place...juice tu elfu 8.....mmmhhh.....Mwambie muende Corner Bar uone vita vya 3 vya dunia,,au sehemu tu ambayo ni nzuri ya kawaida..ooh pale kelele,mara pale sijui vile....Mwanamke ambaye hajali una sh ngapi mfukoni,yeye ana-assume una hela tu za kuunguza...Hawazi how to help her man to SAVE! Gold digger hawezi kuhurumia pochi yako,KAMWE!
5. ANGALIA MA-EX WAKE
Ingawa si jambo zuri kufuatilia past za watu...lakini we fuatilia tu watu wa aina gani amedate nao...mara mwanamuziki...mara babu wa kizungu...mara mcheza mpira...mara movie actor...Jiulize,mbona hamna kajamba nani kwenye listi???That means she is selective...anajua huyu atampa kitu.wewe umeibuka unafanya kazi Bodi ya Misuli tanzania,utampa nini???atakupa mitihani mwenyewe hadi utafeli,maana hauko kwenye trend of men anaowataka
6. LAZIMA AFUATILIE KUJUA UNA MSHAHARA WA SH NGAPI AU UNA ASSET NGAPI
Gold digger lazima akupige maswali haya....Baby kwani mshahara wako sh ngapi????Akijua mshahara anaanza kujiset kupiga mizinga.....Kama mshahara milioni 2 hawezi kuona hatari kuomba laki5 ya ghafla ghafla...Na ukimwambia huna utasikia..Yaani u cant give ur babe even laki5???Kwani ya kwako???ina maana mi sina matumizi yangu??sina wazazi???sina ndugu???sina mipango??yaani we utoke huko tu,naomba laki 5,kaichimbe ardhini kama ni rahisi kupata
7.UTAONA KIPOCHI BAADA YA KUFANYA TUKIO LA BEI MBAYA
Hii ni mbaya kusema lakini ndio ukweli.Msichana wa dizaini hii,hakupi penzi hadi ufanye kitu flani hivi ambacho kimeinvolve hela ndefu sana...Kwa mfano,Ukimnunulia simu ghali,na anajua bei yake....Utapewa penzi kwa sababu anajua imekuuma sana kutoa hiyo hela.....Umempa mtaji wa Biashara uchwara aliyokuomba,anakupa penzi....The whole relationship unakuwa kama unalipia penzi kwa changudoa,na bora hata changudoa coz una-bargain ununue wa elfu 20 au 30 kwa saa,hawa mizinga yao huwa ni bab kubwa,ukitoa hiyo hela lazima jasho likutoke!
Labels:
GARISSA FAAQ MAAQ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment