gsa entertainment

Friday, 12 October 2012

BOBBI KRISTINA BROWN’ AVISHWA PETE YA UCHUMBA

Mwezi wa nane mwaka huu binti wa aliyekuwa mwanamuziki maarufu duniani Whitney Houston anayekwenda kwa jina la Bobbi Kristina Brown alivishwa pete na kaka yake wa kufikia Nick Gordon. Pete hiyo yenye kito cha madini ya ‘sapphire’ kilichozungukwa na chembe za almasi iliyowekwa kidoleni kwa binti huyo, wadaku wameitafsiri kama alama ya uchumba japokuwa wawili hao wamekana wakisema ilikuwa ni zawadi tu. Hata hivyo kipande cha kipindi cha mahojiano cha luninga alichorekodiwa binti huyo mwenye umri wa miaka 19 kinachoitwa The Houstons: On Our Own kidaiwa kuthibitisha kuwa binti huyo anachumbiwa na Gordon. Nick Gordon kijana mwenye miaka 22 amelelewa na hayati Whitney Houston kama mwanae, hivyo ni sawa na kuwa kaka wa Bobbi Kristina Brown ambaye ghafla baada ya kifo cha mwanamuziki huyo wameonyesha kupendana.

No comments:

Post a Comment